Jeshi la Polisi mkoani Songwe linawashikilia watu wanne katika Kijiji cha Ifuko, Kata ya Chang'ombe mkoani humo kwa tuhuma za mauaji ya Nisetasi Dimoso (43), Mwalimu wa Shule ya Sekondari Galula, aliyeuawa shuleni na watu waliofika kuchukua mifugo yao iliyokuwa imezuiwa baada ya kufanya uharibifu.
Waliokamatwa ni Mwigulu Luhende (21), Boniface Mwawa (20), Masanja Kisiwa (30), na Luhende Melani (19).