Rwanda Yatoa Msaada wa Kibinadamu Gaza

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 month ago
rickmedia: rwanda-yatoa-msaada-kibinadamu-gaza-840-rickmedia

Rwanda imetuma misaada ya kibinadamu huko Gaza, ikionyesha mshikamano na raia wa Palestina waliojeruhiwa katika vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas.

Ndege ya Rwandair Cargo iliyokuwa na tani 16 za dawa, chakula na maji, ilitua nchini Jordan ikielekea Gaza siku ya Ijumaa. Msaada huo unatarajiwa kufika Gaza kupitia Misri kutokana na Israel kuzuia uwasilishaji wa misaada ya moja kwa moja kutoka Jordan.

Siku ya Ijumaa Umoja wa Mataifa ulisema umeafiki makubaliano ya lori 20 za awali za msaada kuingia Gaza kupitia kivuko cha Rafah kutoka Misri, ikiwa ni mara ya kwanza kukabidhiwa hivyo tangu vita kuanza Oktoba 7.