#AntonioRudiger na Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) wanachukua hatua za kisheria baada ya nyota huyo wa Ujerumani kuhusishwa na shirika la kigaidi.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Nyota huyo alishare picha akiwa amevalia kanzu na kukaa kwenye Mswala wa kufanyia ibada Akionyesha kidole cha shahada cha mkono wake wa kulia kuelekea angani huku akitoa salamu za Ramadhan kwa kuandika "Mwenyezi Mungu atukubalie saumu na maombi yetu"
Siku ya Jumatatu, #Rudiger alitoa malalamiko ya jinai dhidi ya #Reichelt katika ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Berlin, akidai kupokea matusi au kashfa ya uchochezi wa uasi.
DFB pia iliwasilisha malalamishi na kuripoti tweet ya #Reichelt kwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma kama 'matamshi ya chuki'. BILD pia ilipokea barua kutoka kwa mawakili wa #Rudiger.
Katika barua kwa mhariri mkuu wa BILD #MarionHorn, wanaonya dhidi ya kauli za uchochezi zinazoweza kumdhuru mteja wao.