Loading...

Mwakinyo aitwa Mahakamani, aomba siku 21 kujiandaa

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

7 months ago
rickmedia: mwakinyo-aitwa-mahakamani-aomba-siku-kujiandaa-181-rickmedia

Bondia maarufu nchini, Hassan Mwakinyo, ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu impe siku 21 ili aandae majibu kuhusu kesi ya madai aliyofunguliwa na Kampuni ya PAF Promotion.

Mwakinyo ametoa ombi hilo kupitia Wakili wake, Azadi Athumani, leo Jumatatu Novemba 20, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amiri Msumi, baada ya kuitikia wito wa Mahakama.

Katika kesi hiyo ya madai namba 227/2023, kampuni ya PAF Promotion imewasilisha madai nane, likiwemo la kumtaka bondia huyo kuilipa Sh150 milion ikiwa ni madhara ya jumla waliopata baada ya bondia huyo kushindwa kupanda ulingoni tofauti na mkataba wake aliosaini.

Kampuni hiyo imemfungulia Mwakinyo kesi hiyo baada ya kushindwa kupanda ulingoni katika pambano lililoandaliwa na kampuni hiyo, lililokuwa limepangwa kufanyika Septemba 29, 2023 jiji hapa; kwa kile alichonukuliwa akisema ni waratibu hao kukiuka masharti ya makubaliano.