Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Al Ahly (Ligi ya Mabingwa Afrika) na Mashujaa FC (Kombe la FA), Simba imepata sare ya goli 1-1 dhidi ya Ihefu FC katika Mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Simba ambayo haijapata ushindi katika mechi nne mfululizo za michuano yote imefikisha pointi 46 katika michezo 20, ikiwa nafasi ya tatu, inatarajiwa kucheza dhidi ya Yanga katika mchezo ujao.
Yanga ndiyo inaongoza Ligi ikiwa na pointi 52 katika michezo 20 ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 47 katika michezo 21.