Mwanamuziki kutoka lebo ya WCB Zuchu ameibuka na kukemea vikali mashabiki ambao wanamshindanisha na nguli wa Bongo Fleva , Lady Jay Dee. Zuchu amesema kuwa ushindani huo hauna tija kwenye muziki na ni kuwavunjia heshima wakongwe waliochonga barabara
Zuchu ametanabaisha hayo kupitia Instastory yake baada ya vikundi vya watu mitandaoni haswa Twitter kuanzisha mjadala huo na moja kati ya watu ambao walikuwa wanapinga mjadala huo kwa kumpa nyota tano Lady Jay Dee ni Rapa Wakazi
Zuchu ameandika Ujumbe huu hapa kukemea mashabiki
"HUU NI MJADALA USIO NA MASHIKO NA WAKIJINGA KUWAHI KUTOKEA .LADY JAYDEE NI MOJA KATI YA ROLE MODELS WANGU NAMPA HESHIMA KUBWA SANA SABABU YEYE NI MOJA KATI MIFANO BORA SANA TULIYONAYO KWENYE TASNIA ESPECİALLY MABINTI .KUNISHINDANISHA MIMI NA DADA ZANGU WALIOTENGENEZA NJIA KAMA DADA KOMANDO NI KUIVUNJIA HESHIMA TASNIA .NAKOMESHA MIJADALA HII MARA MOJA"