Loading...

H BABA aona Ayamalize na Harmonize "Nimesamehe kila kitu"

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 week ago
rickmedia: baba-aona-ayamalize-harmonize-nimesamehe-kila-kitu-736-rickmedia

Msanii wa Muziki H Baba ametangaza kumaliza Tofauti zake na Msanii mwenzie Rajab Abdul Kahali (Harmonize) huku akisisitiza kuwa shinikizo hilo limetoka kwa Mama Yake.

H Baba na Harmonize walitofautiana kwa madai ya H Baba kuwa Harmonize alimpiga changalamacho kwenye mauzo ya wimbo waliofanya pamoja wakiwa na Aliwo Longomba #Attitude Miaka Mitatu iliyopita.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa H Baba amesema kuwa ameamua kufikia uamuzi wa kumaliza tofauti zao kwa kusamehe yote yaliyopita.

"Mama H. Kanitamkia Muda huu hapa Nikusamehe #NYADUNDO Kwakuwa Natafuta Kwa Ajili Yake Mama Hamisi Nimesamehe” Kiroho Safi #Attitude iendelee Nimekunjua Asante Mama Angu”

Niwengi Mlimuombea Msamaha @harmonize_tz Mpaka Yeye Mwenyewe Kaja sana #Mwanza Kimyaa Kimyaa Akutane na Mama H. Bahati Mbaya Mama Angu Akuwepo Alikuwa Kwenye Matibabu Namshukuru Mungu Anaendelea Vizuri”

Leo Mama H. kanitamkia Nimsamehe @harmonize_tz Mashabiki, Wasanii, Viongozi Mbalimbali, Wazazi Wake Nimewaskia Nimemsamehe… Kauli ya Mama Angu Mzazi Leo Imenifungua Moyo” Mimi Nimtoto Wakipekee Kwa Mama Angu Nadeka Nimeskia Mama Angu”

Watanzania Mfahamu Kwamba Sisi Watoto Tunaotokea Familia Zakimaskini Tunapambana Kwa Ajili Ya Familia Zetu pia Napambana Kwa Ajili Ya Mama Angu Mzazi “

Kwakuwa Kanitamkia Nami Nimekunjua Nimemsamehe #NYADUNDO

Namshukuru Sana #Mungu Nimesameheeee Kingine Mama H. Kanizuia Kukaa Kimyaa Bila Kutoa Wimbo Ataaakiiii …Kasema Nitoe Wimbo Nashukuru Mama Kunipa Ruksa Ya Wimbo Wako Pendwa Ndio Utoke Wakwanza #H.BABA ft #BARNABAS

kifupi #MUZIKI ft #MWANAMUZIKI Mfalme wa Mwanza Nakuja Shukrani Kubwa iende Kwa Mashabiki Zangu Pamoja na @diamondplatnumz Kunilipia Video Ya Wimbo Huu Pendwa wa MAMA H.

@barnabaclassic Mama H. kakupa Ruksa Upe Jina Wimbo Huu Mpyaa Unaosubiliwa namashabiki Wapenda Mziki Mzuri “ MUNGU NISAIDIE MAADUI WAUPENDE WIMBO HUU“ Producer: @moccogenius

Director: @director_mareys

Location: Mwanza /Dar

Asanteni Woote Team Kazi Nzuri (TEAM MOCCO) #Wazee Wangu Wa Gamboshi Asanteni nipo Tayari Kupambana Afe Kipa Mimi Ntadaka #WIMBO MPYAA LOAD….