Loading...

Prince Harry arithi Mamilioni kwenye Birthday yake ya Miaka 40

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: prince-harry-arithi-mamilioni-kwenye-birthday-yake-miaka-623-rickmedia

Prince Harry ametajirika zaidi baada ya kurithi zaidi ya dola milioni 10 kwenye siku yake ya kuzaliwa alipofikisha miaka 40, kwa mujibu wa gazeti la London Times. Bibi yake mkubwa, Malkia Elizabeth, Queen Mother, aliweka takriban dola milioni 25 kwenye mfuko maalum kwa ajili ya vitukuu vyake mwaka 1994. Harry na kaka yake, Prince William, walipokea urithi huo kwa awamu mbili, wakiwa na miaka 21 na 40.

Katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, Harry alipokea salamu za heri kutoka kwa baba yake, Mfalme Charles III, na kaka yake, Prince William, pamoja na Kate Middleton kupitia mitandao ya kijamii. Picha iliyopostiwa ilimwonyesha Harry akitabasamu akiwa Dublin, huku mke wake, Meghan Markle, akionekana kukatwa kwenye picha hiyo.

Harry, ambaye anaishi Montecito, California, na familia yake, alisema zawadi bora zaidi aliyowahi kupata ni watoto wake wawili, Archie na Lilibet.