Ndoa ya mdau wa Soka Nchini Tanzania Haji Manara na Mwigizaji Zaiylisa imefika kikomo, hii ni kutokana na namna ambavyo wawili hao wamerushiana maneno mtandaoni huku kila mtu akiweka wazi mabaya aliyofanyiwa na mwenzake.
Manara alianza kwa kumwambia Zaiylisa kuwa sio mwanamke mwenye shukurani japo alikutana naye kipindi ambacho hana hata nguo nzuri za kuvaa kwani alikuwa anavaa vipedo tu, ameeleza namna ambavyo alimtoa mtoto wa Zaiylisa shule za kayumba (Shule za Serkali) na kumpeleka shule bora lakini anamwambia Jogoo wake hapandi mtungi.
Zaiylisa naye kwa upande wake amemtuhumu Haji Manara kuwa alikuwa akimtongoza mtoto wa dada yake Zaylisa alikwenda kuwatembelea kipidi cha likizo, anasema kuna muda alikuwa anamshika shika kifua mtoto huyo huku akimtumia elfu 590 mara kadhaa akiwa shule, anasema haji alikuwa akimtongoza mfanyakazi wao wa ndani pia.
Manara alimlaumu Zaiylisa kuwa alikuwa akimnyima chakula mtoto wake na hiyo ndio sababu ambayo inamfanya amuache, huku kwa upande mwigine Zaiylisa amepinga vikali suala hilo na kudai kuwa ndoa ilikuwa ina shida tangu muda mrefu na alidai talaka muda mrefu ila alikataliwa.
Mungu awasaidie wamalize tofauti zao na waache kuvuana nguo mtandaoni.