Loading...

Moto waua wanafunzi 16 Kenya wa Shule ya Hillside Endarasha Kenya

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 week ago
rickmedia: moto-waua-wanafunzi-kenya-shule-hillside-endarasha-kenya-341-rickmedia

Wanafunzi 16 wameripotiwa Kupoteza maisha baada ya ajali ya Moto kutokea katika moja ya Mabweni ya Shule ya Hillside Endarasha iliyopo Kieni, Nyeri Usiku wa kuamkia Septemba 6, 2024.

Msemaji wa Huduma za Polisi Kenya, Resila Onyango amethibitisha tukio hilo na kueleza "Tuna Wanafunzi 16 wamekufa na 14 wamejeruhiwa. Tunachunguza sababu na kuchukua hatua zinazohitajika."

Taarifa zaidi imeeleza Wanafunzi 15 walifariki ndani ya Bweni, mmoja amefariki wakati akipelekwa Hospitali. Aidha, inadaiwa miili mingine inaweza kuongezeka wakati utafutaji ukiendelea.