Loading...

Papa Francis Afunguka "Si Vibaya Kutania Kiuhusu Mungu"

-rickmedia: Rick

Rick

3 months ago
rickmedia: papa-francis-afunguka-si-vibaya-kutania-kiuhusu-mungu-800-rickmedia

Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani Papa Francis amekutana na wachekeshaji kutoka Mataifa 15 Duniani huko Jijini Vatican nchini Italia kwaajili ya kuzungumza kuhusu uzuri wa mwanadamu na kuitangaza amani.

Papa Francis amekutana na wachekeshaji mbalimbali kama Whoopi Goldberg, Jimmy Fallon, Chris Rock, Stephen Colbert. Kwenye mazungumzo yake Papa amesema kuwa "Katika habari na nyakati nyingi za kuhuzunisha mnaweza kuieneza amani. Mnaunganisha watu kwasababu kucheka kunaambukiza."

Papa hakuishia hapo alisema kuwa "Mnapoweza kusababisha tabasamu hata kwa mtu mmoja basi na Mungu naye anatabasamu. Si vibaya kutania kuhusu Mungu ila iwe kwa njia njema"