Loading...

Rais Biden apendekeza Marais Wastaafu wa Marekani waondolewe Kinga

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: rais-biden-apendekeza-marais-wastaafu-marekani-waondolewe-kinga-370-rickmedia

 Rais Joe Biden amependekeza Bunge la ‘Congress’ lipitishe marekebisho aliyoyaita “Hakuna Aliye Juu ya Sheria,” akilenga kuwafutia Kinga ya Kushtakiwa Marais wa zamani kutokana na uhalifu walioufanya wakiwa Madarakani.

Pia, Biden amependekeza Uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu kuhudumu bila ukomo wa muda uondolewe nao wawe na kipindi maalumu cha utumishi kama ilivyofanywa kwa Marais Miaka 75 iliyopita.

Aidha, amesema Bunge lipitishe marekebisho ya Kanuni za Maadili ya Mahakama ya Juu zitakazowataka Majaji kuweka wazi mienendo yao ikiwemo zawadi wanazopewa, kujiepusha na shughuli za Kisiasa na kujiepusha na kesi ambazo wao au wenzi wao wana maslahi nazo.